
Mkuu wa ufuatiliaji wa RVF katika wizara hiyo ya afya Dkt Boly Diop, amesema huku visa 119 vikiwa vimeripotiwa hadi sasa, zaidi katika eneo la kaskazini mwa Senegal lenye mifugo wengi, mlipuko huo unazua wasiwasi kuhusu kuenea zaidi kwa ugonjwa huo.
Senegal yaripoti maambukizi makubwa zaidi ya RVF
Diop ameviambia vyombo vya habari vya ndani kwamba hii ni mara ya kwanza kwa Senegal kurekodi idadi kubwa ya watu walioathirika.
Dk. Merawi Aragaw Tegegne, mtaalam wa magonjwa katika Kituo cha Afrika cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa, amewaambia waandishi wa habari kwamba kunapokuwa na mvua kubwa na mafuriko yanayofuatiwa na jua, kunapaswa kutarajiwa RVF katika siku zijazo na mazingira mazuri kwa wadudu wanaosambaza magonjwa.