Licha ya kuongezeka kwa idadi ya wanawake wanaogundulika kuwa na ugonjwa wa saratani ya matiti, wataalamu wa afya wanasema hata wanaume nao hawako salama, kwani nao wako katika hatari ya kupata ugonjwa huo.

Imeelezwa kuwa baadhi ya sababu zinazochangia wanaume kupata saratani ya matiti ni pamoja na mabadiliko ya vinasaba, matumizi ya pombe kupita kiasi, uzito uliopitiliza na historia ya ugonjwa huo katika familia.

Msikilize Mkurugenzi wa Huduma za Kinga katika Taasisi ya Saratani Ocean Road, Dk. Crispin Kahesa akifafanua zaidi.

#AzamTVUpdates
✍Alpha Jenipher
Mhariri | John Mbalamwezi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *