Kikosi cha dharura cha Ukraine kimefanya juhudi za kuokoa maisha ya watu na kudhibiti moto uliosababishwa na shambulio lililofanywa na Urusi usiku wa kuamkia leo katika mji wa Kyiv.
Tukio hilo limejeruhi watu tisa na kuharibu nyumba pamoja na miundombinu katika maeneo kadhaa ya jiji hilo.
Katika wilaya ya Pecherskyi, moto mkubwa ulizuka katika jengo la makazi na kulazimisha askari wa zimamoto kufanya kazi usiku kucha kuwaokoa wakazi waliokuwa wamekwama ndani. Jumla ya watu 20 waliokolewa wakiwa hai kutoka kwenye jengo hilo lililokuwa likiwaka moto.
Mamlaka za jiji zinasema juhudi za kuzima moto na kurejesha huduma muhimu zinaendelea, huku wakazi wengi wakihimizwa kuwa waangalifu na kufuata maelekezo ya usalama wakati hatari ya mashambulizi zaidi ikiendelea kuwepo.
#AzamTVUpdates
Mhariri | John Mbalamwezi