#HABARI: Serikali ya Israel imethibitisha rasmi kuidhinisha mpango wa kusitisha mapigano katika Ukanda wa Gaza pamoja na mpango wa kuwaachilia mateka, kwa mujibu wa taarifa kutoka ofisi ya Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu.
“Serikali imeidhinisha mfumo wa kuwaachilia mateka wote walio hai na waliopoteza maisha,” imesema taarifa hiyo. Hata hivyo msemaji wa Serikali ya Israel amesema kwamba Jeshi la Ulinzi la Israel (IDF) litajipanga upya katika mstari mpya mara baada ya kuanza kwa usitishaji mapigano, hatua itakayowaacha wakidhibiti takribani asilimia 53 ya Ukanda wa Gaza.
Hatua hii inafungua njia kwa usitishaji mapigano kuanza kutekelezwa. Pia na mwanzo wa mfululizo wa hatua zingine ambazo zitawezesha kuachiliwa kwa mateka katika siku chache zijazo.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
📱Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 📱kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania