Umoja wa Ulaya (EU) unanuia kuongeza uwekezaji wa biashara katika nchi za Kusini, kama sehemu ya mkakati wake wa “Global Gateway” uliozinduliwa mwaka 2021 ili kukabiliana na ushawishi wa China barani Afrika, EU imetangaza Oktoba 9, 2025, huko Brussels.

Imechapishwa:

Dakika 2 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Kongamano la “Global Gateway” kuhusu uwekezaji wa Ulaya barani Afrika lnaafanyika mjini Brussels mnamo Oktoba 9 na 10, 2025. Miradi kadhaa mikubwa barani Afrika inanufaika na msaada wa Umoja wa Ulaya na mpango huu: Lobito Corridor, mradi wa reli unaolenga kuunganisha Zambia na Atlantiki kupitia DRC na Angola ili kuuza nje rasilimali za madini za nchi hizi; Ukuta Mkuu wa Kijani, ambao unapanga kurejesha uoto katika Sahel kutoka Dakar hadi Djibouti; na kuanzishwa kwa kiwanda cha kuzalisha chanjo cha BioNTech.

Kusini mwa Jangwa la Sahara ilikuwa eneo la kwanza kunufaika na uwekezaji huu wa Global Gateway, ikiwa na karibu euro Bilioni 80 katika ufadhili na dhamana.

Siku ya Alhamisi Rais wa Tume ya Ulaya alitangaza nchini Ubelgiji kwamba lengo la euro Bilioni 300 kwa kipindi cha mwaka 2021-2027 tayari limefikiwa na kuweka kizingiti kipya cha euro Bilioni 400.

Huko Brussels, Ursula von der Leyen alitangaza hali halisi ya diplomasia ya biashara. Mtindo unaobadilika unaoathiri kambi zote kuu za kiuchumi, likiwemo bara la Afrika. “Ushuru wa forodha na vikwazo vya biashara vimerudi kama zana za siasa za kijiografia na uchumi wa kijiografia,” alibainidha. “Udhibiti wa mauzo ya nje umekuwa zana ya kuwadhuru washindani na kupata makubaliano.” Mategemeo yanatumiwa kama silaha, ikiwa ni pamoja na yale yanayotokana na uwekezaji usio endelevu wa kigeni ambao umeacha nchi nyingi zikilemewa na madeni yasiyo endelevu.” Ukosoaji ulioilenga China.

“Uwekezaji huu haufai kuchukua nafasi ya utegemezi mmoja na mwingine”

Kutokana na hali hii, Global Gateway inajiwasilisha kama suluhisho mbadala, ikitoa ufadhili uliochanganywa na endelevu. Cyril Ramaphosa, Rais wa Afrika Kusini na mkuu wa sasa wa G20, anatoa wito kwa ushirikiano huu kuendelea. Lakini si bila masharti. “Ni muhimu kwamba uwekezaji mkubwa unaofanywa kupitia Global Gateway uandaliwe kujenga uwezo wa nchi za Afrika na nchi za Kusini mwa Ulimwengu,” amebanisha. “Na uwekezaji huu haufai kuchukua nafasi ya utegemezi mmoja na mwingine. Lazima uwe wa kuleta mabadiliko na kujenga uwezo. Ni lazima uwezeshe nchi za Afrika na nchi za Kusini kufuata njia za maendeleo zinazolingana na hali zao na mahitaji ya raia wao.”

Katika muktadha wa vikwazo vikali kwenye masoko ya fedha na kupungua kwa misaada ya maendeleo, Global Gateway inageukia ubia wa kibinafsi. Jukwaa la kukuza miradi yao na kupata suluhu za ufadhili limezinduliwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *