Spika wa Baraza la Wawakilishi, Zubeir Ali Maulid amesema kuongezeka kwa wawekezaji nchini ni ishara tosha ya serikali kuweka mazingira mazuri ya uwekezaji.
Spika Zubeir ameyasema hayo wakati wa hafla ya uzinduzi wa duka la vifaa vya kieletroniki majumbani vya kampuni ya Hisense amesema hatua hiyo itakuwa chachu ya kuongeza ajira kwa wananchi wa Zanzibar pamoja na kutumia Matumizi ya vifaa hivyo kwa usalama.
Taarifa ya Mtumwa Said