Mgombea Urais wa Tanzania kwa tiketi ya CCM, Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema katika miaka minne ya serikali ya awamu ya sita imeongeza idadi ya leseni kwa wachimbaji wadogo kutoka 332 hadi 1,766.
Akihutubia wananchi wa Maganzo, Kishapu mkoani Shinyanga, amewapongeza wachimbaji wadogo kwa kuchangia asilimia 40 ya pato la madini nchini na kuahidi kuendelea kuendeleza sekta hiyo, kutatua migogoro ya wachimbaji.
✍ @claud_jm
#AzamTVUpdates