Serikali imesema itaendelea kufanya mambo makubwa kwa watu wenye ulemavu ili kuboresha ustawi wao na kuwawezesha kushiriki kikamilifu katika shughuli za maendeleo.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema hayo Jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya kutambua mchango wa Serikali katika kuinua kundi hilo, akibainisha kuwa Serikali imefufua Mfuko wa Taifa wa Watu Wenye Ulemavu na kutoa zaidi ya shilingi bilioni 2.1, ikiwemo ruzuku ya milioni 408 kwa vyama vya watu wenye ulemavu.
Amesema pia Serikali imetoa bilioni 8 kwa vifaa visaidizi kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum na bilioni 16.4 kupitia mikopo ya Halmashauri ili kuwawezesha kujitegemea kiuchumi.
✍ @claud_jm
#AzamTVUpdates