Vyombo vya habari vya Israel vimetangaza kuwa kundi la kwanza la mateka saba limekabidhiwa kwa Shirika la Msalaba Mwekundu.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Kulingana na habari za hivi punde, Eitan Mor, Gali na Ziv Berman, Matan Angrest, Omri Miran, Alon Ohel, na Guy Gilboa-Dalal ndio mateka wa kwanza ambao wameweza kuachiliwa. Hali zao zinasemekana kuwa za kuridhisha na wote wanaweza kutembea bila kusaidiwa na mtu yoyote. Habari hizo zimeibua shangwe kutoka kwa umati uliokusanyika Tel Aviv.

Wakati huo huo Rais wa Marekani Donald Trump alisafiri kwa ndege kuelekea Mashariki ya Kati siku ya Jumapili jioni. Kabla ya kuelekea Misri kuongoza “mkutano wa kilele wa amani” huko Gaza siku ya Jumatatu mchana, Rais wa Marekani atasimama kwa muda mfupi  nchini Israeli Jumatatu asubuhi. Vita katika Ukanda wa Gaza “imekwisha,” alitangaza ndani ya Air Force One.

Kundi la kwanza la mateka saba wa Israel lilikabidhiwa kwa Shirika la Msalaba Mwekundu karibu saa 8:00 saa Israel. Hii ni hatua ya kwanza katika mpango uliowasilishwa na Donald Trump kwa ajili ya kusitisha mapigano katika eneo hilo: kurejea Israel kwa mateka 48, wakiwa hai au wamefariki, ambao bado wanashikiliwa na Hamas kutambatana na kuachiliwa kwa karibu Wapalestina 2,000 wanaoshikiliwa na Israel.

Rais wa Marekani, ambaye alisafiri kwa ndege kuelekea Mashariki ya Kati Jumapili jioni kwa kutumia Air Force One, amewasili nchini Israel Jumatatu asubuhi. Kisha ataelekea Sharm el-Sheikh, Misri, ambako yeye na mwenzake wa Misri, Abdel Fattah Al Sisi, wataongoza “mkutano wa kilele wa amani” huko Gaza Jumatatu mchana. Viongozi kutoka nchi zaidi ya 20 wanatarajiwa kuhudhuria, pamoja na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres. Hata hivyo, hakuna wawakilishi wa Israel watakaohudhuria.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *