
Wakati mateka wa mwisho wa Israel ambao walikuwa bado wanashikiliwa na Hamas wameachiliwa huru leo Jumatatu hii asubuhi, Donald Trump amewasili nchini Israel, ambapo atafanya mapumziko mafupi kabla ya kuelekea Misri kuongoza “mkutano wa amani” huko Gaza. Vita katika Ukanda wa Gaza “imekwisha,” ametangaza ndani ya ndege yake, Air Force One.
Imechapishwa:
Dakika 2 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Hamas imewaachilia mateka 20 wa mwisho waliokuwa wanashikiliwa katika Ukanda wa Gaza leo Jumatatu asubuhi. Kundi la kwanza la mateka saba wa Israel lilikabidhiwa kwa Shirika la Msalaba Mwekundu mwendo wa saa 8 saa za Israel, likifuatiwa na kundi la pili la watu 13. Hatua ya kwanza ya mpango wa Donald Trump wa kusitisha mapigano pia inajumuisha kurejeshwa kwa mabaki ya mateka 28 waliofariki. Kwa kubadilishana, karibu Wapalestina 2,000 wanaoshikiliwa na Israel wataachiliwa.
Rais wa Marekani Donald Trump awasili katika makao makuu ya Knesset mjini Jerusalem
Rais wa Marekani Donald Trump amewasili katika Knesset, bunge la Israel mjini Jerusalem, ambako ameratibiwa kutoa hotuba, kwa mujibu wa ripota wa shirika la habari la Agence France-Presse (AFP). “Hii ni heshima kubwa kwangu, siku kuu, siku nzuri sana. Mwanzo mpya,” ameandika katika kitabu cha wageni cha Knesset, huku Spika wa Bunge Amir Ohana na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu wakitazama.
Rais wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina Mahmoud Abbas kuhudhuria “Mkutano wa Amani” nchini Misri
Rais wa Palestina Mahmoud Abbas atahudhuria “mkutano wa kilele wa amani” kuhusu Gaza utakaofanyika leo Jumatatu nchini Misri, Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron ametangaza. Mkutano huu unaosimamiwa na Rais wa Marekani Donald Trump na Rais wa Misri Abdel Fattah Al Sisi, utawaleta pamoja zaidi ya viongozi 20 kusherehekea usitishaji vita huko Gaza na kurejea kwa mateka wa Israel kwa kubadilishana na wafungwa wa Kipalestina. Abbas ni mpinzani wa Hamas, ambapo shambulio lake dhidi ya Israeli mnamo Oktoba 7, 2023, lilianzisha vita huko Gaza. Israel wala Hamas hawatawakilishwa kwenye mkutano huo.
EU kuanza upya misheni ya ufuatiliaji katika kivuko cha mpaka cha Rafah siku ya Jumatano
Umoja wa Ulaya utaanza upya ujumbe wake wa ufuatiliaji katika kivuko cha mpaka cha Rafah kati ya Gaza na Misri “siku ya Jumatano,” mkuu wa sera za kigeni wa Umoja wa Ulaya Kaja Kallas ametangaza katika ujumbe kwenye mtandao wa kijamii wa X. Ujumbe wa ufuatiliaji wa EUBAM, unaohusisha vikosi vya polisi vya Italia, Uhspania, na Ufaransa, unalenga kuhakikisha uwepo wa upande wowote, wa tatu katika kivuko hiki cha mpaka huu wa kimkakati. Ulitumwa mnamo mwezi Januari, kabla ya kusitishwa mwezi Machi.
EU inakaribisha kuachiliwa kwa mateka wa Israel, “hatua iliyowezeshwa na Rais Trump”
Waziri wa Mambo ya Nje wa Umoja wa Ulaya Kaja Kallas amekaribisha kuachiliwa kwa mateka saba wa Israel walioachiliwa huru na Hamas siku ya Jumatatu, akisisitiza jukumu la Rais Trump katika “hatua hii muhimu kuelekea amani.” “Kuachiliwa kwa mateka ni mafanikio makubwa kwa diplomasia na hatua muhimu kuelekea amani. Rais Trump amefanikisha hatu hii,” amesema kwenye mtando wa kijamii wa X.