Mgombea Urais wa Tanzania kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Samia Suluhu Hassan amewataka vijana nchini humo, kuonesha uzalendo kwa nchi yao, waipende, walinde amani yake na kutokukubali kushawishiwa kuharibu amani hiyo.
“Vijana nawaomba tuwe wazalendo, tuipende nchi yetu. Hatuna nchi nyingine isipokuwa Tanzania, msije kuruhusu mtu akaja akasema fanyeni hili, fanyeni hivi. Sisi tunaipenda nchi yetu, nanyi muipende nchi yenu na muwe wazalendo,” alieleza Samia, ambaye pia ni Rais wa Tanzania, wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika wilayani Bukombe mkoani Geita.
Kulingana na Samia, kuna nchi mmoja tu duniani, iitwayo Tanzania, na toka kuundwa kwake, imepigana vita dhidi ya Idi Amin peke yake.
Samia aliongeza kuwa, nchi hiyo imebakiwa kuwa salama kwa miaka mingi, huku watu wan chi hiyo wakiendelea kuilinda tunu hiyo.