#HABARI: Jeshi la Polisi mkoani Songwe linamshikilia Justine Gama (40), Raia wa Malawi anayeishi mjini Mzuzu, kwa tuhuma za kukutwa na vipande 15 vya pembe za ndovu kinyume na Sheria za Uhifadhi wa Wanyamapori.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe, Augustino Senga, mtuhumiwa alikamatwa Oktoba 11, 2025 saa 4:30 usiku katika Kitongoji cha Kabwe, Wilaya ya Ileje, akiwa amevificha vipande hivyo kwenye mifuko ya salfeti ili kukwepa kukamatwa.

Uchunguzi wa awali umebaini kuwa Gama alikuwa na nia ya kusafirisha pembe hizo nje ya nchi.

Kamanda Senga amesema Jeshi la Polisi litaendelea kushirikiana na mamlaka za uhifadhi kuhakikisha wote wanaojihusisha na biashara haramu ya pembe za ndovu na bidhaa nyingine za wanyamapori wanakamatwa na kufikishwa mbele ya vyombo vya sheria.

Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

📱Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 📱kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *