
Katika taarifa, Iran imesema wito huo unakinzana tabia ya kihalifu inayooneshwa na Marekani kwa watu wa Iran.
Wakati wa hotuba yake katika bunge la Israel, Knesset, hapo jana Rais Trumpalisema anataka makubaliano ya amani na Iran na kwamba kwa makubaliano yoyote kupatikana itategemea Iran yenyewe.
“Na kwa Iran kama mnavyojua, hili halisemwi kutokana na unyonge,hakuna unyonge ila nitasema hivi, tuko tayari nyie mkiwa tayari, na utakuwa uamuzi bora zaidi ambao umewahi kufanywa na Iran, na utafanyika.”
Trump pia alisema itakuwa vyema kama Iran itawacha kuwaunga mkono magaidi, isite kuwatishia majirani zake na iwache kuwafadhili wanamgambo wake na pia itambue haki ya uwepo wa Israel.
Tehran ilimjibu Trump kwa kusema matamshi yake ni ya ovyo na ya kutia aibu.