#HABARI: Aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalumu mkoa wa Arusha Cecilia Paresso, amewataka wananchi wa Mkoa wa Kigoma kuwachagua wagombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), kwasababu imewaleta wagombea wenye sifa za kuwaletea maendeleo.

Akizungumza kwenye mkutano wa mgombea Mwenza wa CCM Dkt.Emmanuel Nchimbi jimbo la Kigoma Kaskazini, amewataka kujitokeza kwa wingi Oktoba 29,2025 kuwachagua viongozi wa CCM.

“Chama chetu kimetuletea wagombea wenye sifa na wenye uwezo na kimejipanga kushinda kwasababu ambazo nimezieleza,”amesema Paresso

Kada huyo wa CCM ni miongoni mwa wanachama wa chama hicho wanaomtafutia kura mgombea urais wa CCM,Dkt.Samia Suluhu Hassan,wagombea ubunge na udiwani nchini.

Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

📱Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 📱kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *