#HABARI: Serikali ya Kenya imetangaza siku saba za maombolezo ya Kitaifa na Bendera kupeperushwa nusu mlingoti, katika maeneo yote ikiwemo balozi zote za Kenya, kufuatia kifo cha Waziri Mkuu Mstaafu Raila Hayati, pia Bendera zitapepea nusu mlingoti.

Rais William Ruto amemuomboleza Raila Odinga na kiongozi wa chama cha ODM kama mpiganiaji shupavu wa demokrasia, katika hotuba ya moja kwa moja kutoka ikulu, Rais Ruto amemtaja Raila kama kiongozi aliyekuwa na maono makubwa kwa ukuaji wa taifa la kenya.

Kundi la Viongozi wakuu serikalini wakiongozwa na Waziri wa mambo ya nje Musalia Mudavadi pamoja na mawaziri, wanaelekea India kuurejesha nyumbani mwili wa marehemu Hayati Raila Odinga

Rais William Ruto amewaomba wakenya ,kuiga mfano mwema wa Raila na kuishi maono yake

•Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

📱Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 📱kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *