Kufuatia harakati za vuguvugu za chini chini za Raila Odinga, kuweka kidole wakati hasa alianza kujiingiza katika siasa za Kenya ni ngumu, kwani mbele ya macho anaonekana maisha yake yote tangu ujanani amekuwa akijihusisha.

Lakini katika miaka ya 1980-1990, aliibuka kama mwana mageuzi mkubwa akipigana na ukabila, utawala wa mapendeleo na ukandamizaji wa demokrasia kupitia chama kimoja.

1982: Raila Odinga, mtoto wa Makamu wa kwanza wa Rais wa Kenya Jaramogi Oginga Odinga, alizuiliwa na maafisa wa utawala baada ya kuhusishwa na jaribio la mapinduzi lililoshindwa dhidi ya serikali ya Rais Daniel arap Moi.

Kuna simulizi zinazokinzana juu ya matukio yaliyofuata, lakini licha ya kuzuiliwa kwa muda, Raila aliachiliwa huru huku baadhi ya waliothibitishwa kufanya jaribio la mapinduzi wakiadhibiwa vikali wakiwemo maafisa 3000 wa jeshi la wana anga na raia.

Miongoni mwa washirika wa karibu wa Raila Odinga waliohukumiwa kifo ni Ezekiah Ochuka na Pancras Oteyo Okumu, waliokuwa wakuu wa jeshi la wanamaji.

1988–1991: Baada ya tukio la 1982, Raila Odinga aliongeza kasi katika harakati zake kama mhusika mkuu katika vuguvugu la kuunga mkono demokrasia nchini Kenya, akisukuma mageuzi ya vyama vingi.

1992: Siasa za vyama vingi vyarejea. Raila anajiunga na chama cha baba yake, FORD-Kenya, kuashiria kuingia kwake rasmi katika siasa za uchaguzi.

2002: kufikia uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi nchini Kenya, Raila Odinga alijikuta na umati wa wanasiasa wa upinzani jukwaani ambao wanashukuriwa kwa pamoja kwa juhudi zao za kusukuma demokrasia. Aliamua kumuunga mkono Kibaki na pamoja wakaunda chama cha Liberal Democratic Party (LDP) baada ya kuachana na KANU. Baadaye waliunda muungano wa vyama vingi ujulikanao kama Rainbow Coalition, bendera waliopepea nao katika uchaguzi wa 2002.

Japo watu wengi walimuona kama mmoja wa wagombea wenye nguvu zaidi kuwania urais, Raila Odinga aliwashangaza wengi alipotoa Kauli ya ‘Kibaki Tosha.’

Hii ilionyesha sura nyingine ya Raila ambayo ilichambuliwa na wengi kama azma ya kiukweli ya kuleta mageuzi, hata kama inamaanisha kumuachia mwanasiasa mwenza kushikilia madaraka. Kibaki akashinda uchaguzi huo.

Lakini ghafla mipasuko ilitokea ndani ya muungano huo, na kuweka msingi wa azma ya Raila mwenyewe ya urais.

2007: Ukawa mwaka wa kwanza kwa Raila Odinga kujaribu kuwania urais chini ya bendera ya Orange Democratic Movement (ODM) dhidi ya Rais Kibaki.

Uchaguzi huo umekumbwa na madai ya wizi wa kura na ghasia za baada ya uchaguzi na kusababisha vifo vya zaidi ya watu 1,000.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *