Chanzo cha picha, Reuters
Umoja wa
Falme za Kiarabu umeionya Israel kwamba kutwaa Ukingo wa Magharibi unaokaliwa
kwa mabavu ” kutavuka mpaka” na kudhoofisha ari ya Mkataba wa Abraham
ambao ulirejesha uhusiano kati ya nchi hizo mbili.
Afisa mkuu
wa Imarati, Lana Nusseibeh, alisema hatua hiyo itakuwa mwisho wa kutafuta
suluhisho kwa mataifa hayo mawili katika
mzozo wa Israel na Palestina.
Wizara ya
mambo ya nje ya Mamlaka ya Ndani ya Palestina imesema inakaribisha msimamo wa
UAE.
Serikali ya
Israel haijatoa maoni yoyote. Lakini matamshi ya Nusseibeh yalikuja baada ya
Waziri wa Fedha mwenye msimamo mkali Bezalel Smotrich kufichua pendekezo la
kutwaliwa kwa takriban theluthi nne za Ukingo wa Magharibi.
Israel
imejenga takriban makazi 160 ya Wayahudi 700,000 tangu ilipoikalia kwa mabavu
Ukingo wa Magharibi na Jerusalem Mashariki – ardhi ambayo Wapalestina wanataka,
pamoja na Gaza, kwa taifa linalotarajiwa – wakati wa vita vya Mashariki ya Kati
vya 1967. Takriban Wapalestina milioni 3.3 wanaishi kando ya eneo hilo..
Makazi hayo
ni kinyume cha sheria chini ya sheria za kimataifa.