#HABARI: Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mikoa ya Lindi na Mtwara limezindua rasmi mtambo wa kuzalisha umeme kwa kutumia gesi asilia wenye uwezo wa megawati 20 katika Kituo cha Mtwara II, uzinduzi huu ni hatua muhimu katika utekelezaji wa mkakati wa Serikali ya Awamu ya Sita wa kuhakikisha upatikanaji wa nishati ya uhakika, nafuu na endelevu nchini.

Uwekezaji huu umeongeza uwezo wa kituo hicho kutoka megawati 57.5 hadi kufikia megawati 77.5 na hivyo kulifanya eneo la Kusini liwe na ziada ya umeme kwa mahitaji ya viwanda, biashara na ajira mpya kwa wananchi kujiajiri katika biashara.

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi, Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Mhe. Kanali Patrick Sawala, ametoa shukrani kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutoa kipaumbele kwa uwekezaji kwenye miradi ya nishati inayowanufaisha wananchi wa Kusini.

“Tuna kila sababu ya kumpongeza na kumshukuru Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutuongezea mtambo huu wa kuzalisha umeme. Hii ni hatua muhimu katika kuinua maisha ya wananchi wetu na kuchochea maendeleo ya viwanda katika mikoa ya Lindi na Mtwara,” alisema Mhe. Sawala.
Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

📱Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 📱kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *