#HABARI: Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni mgombea Ubunge wa Jimbo la Karagwe, Innocent Bashungwa, amewahakikishia Watanzania wote kuwa ulinzi na usalama umeimarishwa nchi nzima, hivyo wananchi wajitokeze kwa wingi kushiriki kupiga kura kuwachagua Rais, Wabunge na Madiwani bila hofu yoyote kesho Oktoba 29, 2025.

Bashungwa ameyasema hayo leo wakati wa mkutano wa kufunga kampeni za Chama Cha Mapinduzi (CCM) kitaifa, ikiwa ni siku moja kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2025.

“Kesho, Oktoba 29, hakutakuwa na shida yoyote. Vyombo vya usalama vilivyo chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani, kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi, vipo timamu nchi nzima. Usalama umeimarishwa, kwa hiyo Watanzania tuende tukapige kura bila kuwa na wasiwasi wowote. Na yeyote atakayethubutu kuvuruga amani, atakutana na kisiki,” amesisitiza Bashungwa.

Aidha, Bashungwa ametoa wito kwa vijana kujitokeza kushiriki kikamilifu katika uchaguzi huo, akiwataka pia kujiepusha na vitendo au vishawishi vyovyote vinavyoweza kuvuruga amani, akisisitiza kuwa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi imebainisha fursa nyingi mahsusi kwa ajili ya vijana.

Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

📱Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 📱kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.
Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

📱Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 📱kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *