
Baada ya siku kadhaa za kukosekana kwa mitandao nchini Tanzania, huduma hizo zimerejea saa chache baada ya kuapishwa kwa Rais Samia Suluhu Hassan, Jumatatu ya Novemba 3, 2025.
Huduma hizo zilizitishwa kufuatia kuibuka kwa vurugu na maandamano yaliyozuka sehemu mbali mbali za nchi hiyo wakati wa Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29.
Watu kadhaa wanahofiwa kupoteza maisha na wengine kujeruhiwa, huku mali na miundombinu ikiharibiwa wakati wa vurugu wa za baada ya uchaguzi huo.