
Haya ni licha ya jeshi la polisi nchini humo kuonya kupitia jumbe wa simu za mkononi uliotumwa kwa wananchi kuwa usambazaji wa picha na video kama hizo ni kosa la jinai.
Upinzani nchini humo ambao unapinga uchaguzi uliompa Rais Samia Suluhu ushindi wa asilimia 98, unasema kuwa mamia ya watu waliuwawa.
Huduma za intaneti zimeanza kurejea ingawa imekuwa vigumu kuthibitisha taarifa kutoka taifa hilo la Afrika Mashariki.
Mwandishi wa shirika la habari la Ufaransa AFP amesema hali ya kawaida imeanza taratibu kurejea katika mji mkuu wa kibiashara wa Dar es Salaam ingawa watu wanaonekana kuwa na hofu bado na maafisa wachache wa ulinzi wameonekana katika mitaa ya mji huo.