Urusi: Vikosi vyetu vinazidi kusonga mbele UkraineUrusi: Vikosi vyetu vinazidi kusonga mbele Ukraine

Kamanda mkuu wa jeshi la Ukraine Oleksandr Syrskyi, ambaye amekadiria kwamba Urusi ina zaidi ya wanajeshi 100,000 wanaopigana katika eneo hilo, anasema vikosi vyake vinajitahidi kuwaondoa wanajeshi wa Urusi na kudumisha udhibiti wao.

Pokrovsk ni kitovu cha miundo mbinu ya barabara na reli katika eneo la mashariki la Ukraine la Donetsk ambacho kabla ya vita kilikuwa na wakazi takriban 60,000.

Watu wengi sasa wamekimbia eneo hilo, watoto wote wamehamishwa na raia wachache kusalia licha ya majengo ya ghorofa yalioharibiwa na barabara zenye mashimo.

Mgodi wa pekee wa Ukraine unaozalisha makaa ya mawe yaliotumika katika iliyokuwa sekta kubwa ya chuma, uko umbali wa kilomita 10 magharibi mwa Pokrovsk.

Mnamo mwezi Januari, kampuni ya kutengeneza vyuma ya Ukraine, Metinvest, ilisema imesitisha shughuli za uchimbaji katika eneo hilo.Mji huo pia uko kwenye barabara kuu ambayo imekuwa ikitumiwa na jeshi la Ukraine kusambaza vifaa kwa kambi nyingine zilizozongwa na vita.

Chuo kikuu cha kiufundi huko Pokrovsk, kikubwa na kikongwe zaidi, kimetelekezwa na kuharibiwa kwa makombora.

Urusi inataka kuliteka eneo lote la Donbas, ambalo linajumuisha mikoa ya Luhansk na Donetsk. Ukraine bado inadhibiti karibu 10% ya Donbas – eneo la kilomita za mraba 5,000 magharibi mwa Donetsk.

Je, kudhibitiwa kwa mji huo kuna maana gani?

Kukamatwa kwa Pokrovsk, iliyopewa jina la “lango la Donetsk” na vyombo vya habari vya Urusi, na Kostiantynivka katika eneo la kaskazini mashariki ambalo vikosi vya Urusi pia vinajaribu kuzingira , kunaweza kutoa fursa kwa Moscow kuelekea kaskazini katika miji miwili mikubwa iliyo chini ya udhibiti wa Ukraine huko Donetsk – Kramatorsk na Sloviansk.

Mwananjeshi wa Urusi akiwa katika uwanja wa vita nchini Ukraine.
Mwananjeshi wa Urusi akiwa katika uwanja wa vita nchini Ukraine.Picha: Alexander Polegenko/picture alliance

Pia itaipa Urusi ushindi wake muhimu zaidi na wa kipekee wa kieneo tangu ilipouteka mji ulioharibiwa wa Avdiivka mapema mwaka  2024.

Rais wa Urusi Vladimir Putin amesema kisheria, Donbas sasa ni sehemu ya Urusi. Ukraine na mataifa mengi ya Magharibi yamesema yanapinga hatua ya Urusi ya kuliteka eneo hilo na kuitaja kuwa unyakuzi haramu wa ardhi.

Baadhi ya wachambuzi wa kijeshi wa Magharibi, kama Rob Lee, mfanyakazi mkuu katika

Taasisi ya Utafiti wa Sera ya Kigeni yenye makao yake makuu nchini Marekani, amesema kukamatwa kwa Pokrovsk kutaipa Urusi ushindi muhimu, haswa ikiwa inaweza kufanya hivyo ifikapo mwisho wa mwaka.

Ijapokuwa ni muhimu kwa sababu za utendaji, Lee anasema kuuteka mji wa Pokrovsk bado kutaiwacha Urusi na kazi nyingi ya kufanya linapokuja suala la kuchukuwa udhibiti wa maeneo mengine ya Donetsk na miji miwili muhimu ya Kramatorsk na  Sloviansk.

Hata hivyo Ukraine imechukuwa hatua za haraka za kuimarisha nafasi yake mjini humo.

Zelensky: Mapigano makali yanaendelea

Siku ya Jumapili, rais wa nchi hiyo Volodymyr Zelensky alisema kuna mapigano makali mjini humo na maeneo ya kuuelekea, huku ikiwa vigumu kufanya mipangilio. Hata hivyo ameongeza kusema lazima waendelee kuwaangamiza wavamizi.

Ukraine yarusha makombora ya ATACMS kuelekea Urusi

To view this video please enable JavaScript, and consider upgrading to a web browser that supports HTML5 video

Kwa upande wake, mkuu wa jeshi la Urusi Valery Gerasimov, amemwambia rais wa nchi hiyo Vladimir Putin kwamba Urusi imezuia idadi kubwa ya wanajeshi wa Ukraine katika eneo hilo.

DeepState, jukwaa la kidijitali linalotumia picha zilizothibitishwa kutoka vyanzo huru kutoka uwanja wa vita, linaonyesha kuwa vikosi vya Urusi vinaelekea mjini humo.

Hata hivyo, jukwaa hilo limeeleza kwamba sehemu kubwa ya mji huo hauko chini ya udhibiti kamili wa upande wowote

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *