Taarifa hiyo ni kulingana na mashirika ya misaada wakati Ofisi ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa imeonya kuwa bado kuna watu wengi waliokwama kwenye mji huo.

Taarifa ya mashirika ya misaada iliyotolewa Jumamosi imeongeza kuwa watu wanaofanikiwa kufika katika kambi ya Tawila, kilometa 70 kutoka el Fasher hawana mahema ya kutosha na wanatumia maturubai na mashuka yaliyochakaa.

Watu wasiopungua 16,000 wamekimbilia Tawila

Zaidi ya watu 16,200 wamelazimika kukimbilia katika makambi kwenye eneo la Tawila tangu wanamgambo wa RSF walipoudhibiti mji wa El Fasher kwa mujibu wa shirika la Sudan linalowasaidia wakimbizi wa ndani na kuendesha shughuli za misaada katika kambi za wakimbizi.

Aidha, Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM linakadiria kuwa takriban watu 82,000 wameukimbia mji huo na maeneo jirani tangu Novemba 4 na kuelekea kwenye sehemu salama ikiwemo Tawila.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *