
Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS imetangaza kuwa safari ya rais wa utawala ghasibu wa kizayuni katika nchi za Afrika ni jaribio la kutaka kubadilisha msimamo wa nchi hizo wa zinazopinga ukoloni na kuunga mkono haki za watu wa Palestina.
Kulingana na Kwa mujibu wa televisheni ya Al-Mayadeen, Rais wa utawala wa kizayuni wa Israel Isaac Herzog anatarajiwa kuzitembelea Zambia na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, ambazo wananchi wake wanaunga mkono haki za watu wa Palestina.
Chaneli ya i24 News imetangaza kuwa, katika juhudi za kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia kati ya utawala wa kizayuni na nchi za Afrika, Herzog leo Jumatatu atazitembelea Zambia na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo, Herzog atakuwa rais wa kwanza wa utawala wa kizayuni kuitembelea Zambia. Imeelezwa kuwa, safari yake hiyo itachukua muda wa siku moja kuzitembelea nchi zotehizo mbili.
Safari hii inafanyika wakati ambapo rais huyo wa utawala wa kizayuni anaonekana kulipa umuhimu maalumu suala la kupanuliwa uhusiano wa Tel Aviv na nchi za bara la Afrika.
Ziara hiyo inafuatia kufunguliwa tena ubalozi wa Israel nchini Zambia. Wakati wa ziara hiyo, Herzog atakutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Zambia Hakainde Hichilema na Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Felix Tshisekedi pamoja na maafisa wengine waandamizi wa nchi hizo.
Kwa mujibu wa vyanzo rasmi, mikutano ya kisiasa atakayofanya rais wa utawala wa kizayuni wakati wa safari yake hiyo itajikita kwenye masuala kadhaa zikiwemo changamoto za kimataifa, kuimarisha nafasi ya Tel Aviv katika uga wa kimataifa, kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia na nchi wenyeji, na kupanuliwa ushirikiano wa kikanda na kimataifa…/