#HABARI: Vyama vya siasa 6 vimewasilisha majina ya wagombea wa nafasi ya Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, katika uchaguzi wa Spika unaotarajiwa kufanyika Novemba 11, 2025, ambao wote wameidhinishwa kwa kukidhi vigezo vya kuwania nafasi hiyo.

Taarifa kwa Umma iliyotolewa na Katibu wa Bunge Bw. Baraka Leonard imesema hadi kufikia saa kumi Alasiri Novemba 10, wagombea waliowasilishwa na vyama vyao ni Mh. Mussa Azzan Zungu kutoka (CCM), Yeronika Charles Tyeah kutoka NRA na Anita Alfani Mgaya wa Chama cha NLD.

Wengine ni Chrisant Nyakitita kutoka DP, Ndonge Saidi Ndonge kutoka AAFP na Amin Alfred Yango kutoka ADC.

Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

📱Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 📱kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *