Wananchi wa Kitongoji cha Kanisani, wilayani Mvomero mkoani Morogoro, wanakabiliwa na uhaba wa maji safi na salama, hali inayowalazimu kutumia maji kutoka bwawa linalotumiwa pia na wanyama mbalimbali.
Wanasema kukosekana kwa chanzo cha uhakika cha maji kumeathiri afya zao na shughuli za kila siku, huku wakiiomba serikali kuwapatia huduma ya maji safi haraka.
#AzamTVUpdates
Mhariri | John Mbalamwezi