Wadau wa kilimo wamezitaka serikali za Tanzania, Kenya na Uganda kutimiza malengo ya sera za kilimo misitu ili kuwasaidia wananchi wa nchi hizo kuondokana na umaskini na kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi.
Wametoa wito huo wakati wa uzinduzi wa kongamano la 10 la kilimo misitu, ambapo wamebainisha kuwa utekelezaji thabiti wa sera hizo unaweza kuongeza tija, kulinda mazingira na kuchochea maendeleo endelevu katika jamii.
#AzamTVUpdates
✍Augustine Mgendi
Mhariri | John Mbalamwezi