#HABARI: Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam Novemba 25, mwaka huu inatarajia kutoa uamuzi mapingamizi mawili yaliyowasilishwa na mawakili wa upande wa utetezi kwa watuhumiwa 22 waliopanga na kuhamasisha maandamano ya kuzuia Uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 29, 2025 ikiwemo uhalali wa mashtaka mawili na hoja ya ubovu wa hati ya mashtaka.

Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Mh. Aaron Lyamuya ameyasema hayo baada ya kusikiliza hoja za mawakili wa upande wa Jamhuri wakioongozwa na Wakili Mwandamizi wa Serikali Hemed Khalfan aliyeomba Mahakama kutupilia mbali hoja ya kupigwa na kujeruhiwa kwa watuhumiwa wakilazimishwa wasaini maelezo yanayosemekana kuwa ni ya onyo na kusema hoja hiyo sio wakati wake na Wakili Peter Kibatala amesikia maneno tu na hakushuhudia jambo hilo na kuomba Mahakama kuikataa hoja hiyo.

Katika kesi hiyo yenye watuhumiwa 22 ambayo imesikilizwa kwa njia ya video, waliopanga na kuhamsisha maandamano ya kuzuia Uchaguzi Mkuu alikuwemo mfanyabiashara Jeniffer Jovin Bilikwija maarufu kama ‘Niffer’.

Wakili huyo mwandamizi wa Serikali Hemed Khalfan amedai mpaka sasa hakuna malalamiko ya watuhumiwa kuhusu kufanyiwa ukatili na kupigwa hivyo anashangaa hoja hizo kuwasilishwa Mahakamani hapo.

Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
-📱Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 📱kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *