Waziri wa Viwanda na Biashara, Judith Kapinga amesema taasisi zote zilizo chini ya wizara yake zinapaswa kujikita kwenye uchumi shindani wa viwanda kwa kuongeza ubunifu na ufanisi, ili kuzalisha bidhaa bora zinazokidhi viwango vya kimataifa.

Akizungumza wakati wa ziara aliyoifanya katika Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Kapinga alibainisha kuwa kuimarishwa kwa mifumo ya viwango na teknolojia kutasaidia bidhaa za ndani kushindana kimataifa na kuchochea ukuaji wa uchumi wa taifa.

#AzamTVUpdates
✍Upendo Michael
Mhariri | John Mbalamwezi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *