
Rais wa Marekani Donald Trump, amesema, anatoa onyo la mwisho kwa kundi la Hamas, na kuwataka wakubali mkataba utakaosababisha kuachiwa huru kwa mateka wote.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Kupitia chapisho lake, aliloandika kupitia mitandao ya kijamii, rais Trump ametoa onyo hilo, bila kufafanua zaidi, kitakachofuata iwapo, Hamas watakubali mkataba huo.
Aidha, Trump ameitaka Israeli kukubali masharti ya Marekani kuhusu usitishwaji wa vita vinavyoendelea. Trump alitoa onyo kama hili pia mapema mwezi Machi, alipotaka kuachiwa huru kwa mateka wote wanaoshikiliwa na Hamas.
Israel inasema mateka 47 bado wako mikononi mwa Hamas, wakiwemo 25 ambao wameuawa.
Marekani imekuwa ikiifanyia kazi mkataba mpya wa kusitisha vita, lakini haujawekwa wazi.
Wakati Trump akitoa onyo hilo, jeshi la Israeli limeendelea kutekeleza mashambulio mazito kwenye mji wa Gaza, likiwemo jengo la Al-Ruya na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 60.