Hamas imesema siku ya Jumapili Septemba 7 kwamba iko tayari kuanza tena mazungumzo “mara moja” baada ya kupokea pendekezo jipya kutoka Washington. Donald Trump ametuma “onyo la mwisho” kwa Hamas kwa kurejea kwa mateka wa Israel wanaoshikiliwa katika Ukanda wa Gaza. Hamas inashutumiwa na jeshi la Israel, ambalo linazidisha operesheni zake kwenye mji wa Gaza. Jeshi la Israel limeharibu jengo refu jingine, ambalo ni la tatu katika siku tatu.

Imechapishwa:

Dakika 2 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

“Tumepokea, kupitia wapatanishi, baadhi ya mawazo kutoka kwa Marekani kufikia usitishaji vita huko Gaza, na Hamas inathibitisha utayarifu wake wa kuketi mara moja kwenye meza ya mazungumzo,” Hamas imeandika katika taarifa yake.

Hapo awali, Rais wa Marekani Donald Trump alitangaza kuwa ametuma “onyo la mwisho” kwa Hamas kuhusu kurejea kwa mateka wa Israel wanaoshikiliwa katika Ukanda wa Gaza, akidai kuwa “ameonya” kundi hilo lenye silaha “juu ya madhara ikiwa litakataa.” “Israel imekubali masharti yangu. Ni wakati wa Hamas kukubali pia. Hili ni onyo langu la mwisho, hakutakuwa na lingine,” rais wa Marekani ameandika kwenye mtandao wake wa Truth Social.

Kuongezeka kwa operesheni huko Gaza

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu ametangaza siku ya Jumapili, Septemba 7, upanuzi wa operesheni za kijeshi ndani na karibu na Gaza, na kusema kwamba takriban watu 100,000 tayari wameondoka eneo hilo. Kulingana na makadirio ya hivi karibuni ya Umoja wa Mataifa, karibu watu milioni moja wanaishi ndani na karibu na jiji hilo. Si jeshi wala serikali ya Netanyahu iliyotangaza rasmi kuanza kwa mashambulizi makubwa dhidi ya mji wa Gaza, yaliyoidhinishwa mwezi Agosti, kwa lengo lililowekwa la kuchukua udhibiti wa mji huo, kuwashinda Hamas, na kuwaachilia mateka wanaoshikiliwa tangu Oktoba 7.

Hata hivyo, katika wiki za hivi karibuni, jeshi la Israel limezidisha mashambulizi yake ya mabomu na operesheni za ardhini ndani na karibu na mji huo, ambao wanauonyesha kama ngome ya mwisho ya Hamas, lakini ambayo pia inadai kuwa sasa inadhibiti 40%. Mnamo Septemba 7, jeshi la Israel lilishambulia kwa mabomu jengo jingine refu katika Jiji la Gaza, la tatu katika siku tatu. Mashahidi wameripoti kuwa jengo hilo liliharibiwa katika shambulio, ambalo ulimesababisha kifo cha mtu mmoja, kulingana na Shirika la Ulinzi wa Raia wa Gaza.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *