#HABARI: Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Profesa Palamagamba Kabudi, amewasisitiza viongozi wanaostaafu, kuandika vitabu vinavyoainisha safari za maisha yao, ili kuweka kumbukumbu sahihi za mchango walioutoa kwa taifa na kutoa elimu kwa kizazi kipya.

Amesema hatua hiyo itawawezesha vijana wanaotamani kuwa viongozi kujifunza kupitia uzoefu, changamoto na mafanikio ya waliotangulia.

Profesa Kabudi ametoa rai hiyo wakati akizungumza kuhusu kitabu kipya kilichoandikwa na Balozi mstaafu wa Tanzania nchini Nigeria, Mheshimiwa Daniel Olle Njolai, kitabu kinachoelezea historia ya safari yake ya maisha kuanzia shule ya msingi, taaluma, utumishi serikalini hadi kustaafu, pamoja na namna alivyozikabili changamoto mbalimbali katika uongozi.

Kwa upande wake, Balozi Mstaafu Daniel Njolai amesema ameamua kuandika kitabu hicho ili kiwe mwongozo na rejea muhimu kwa vijana wanaopata nafasi za uongozi, na kwa jamii kwa ujumla, akisisitiza kuwa uzoefu wa viongozi wastaafu ni hazina isiyopaswa kupotea.

Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *