Waziri wa Uchumi wa Buluu na Uvuvi Zanzibar, Masoud Ali Mohamed amesema serikali imefikia hatua ya kufanya maamuzi makubwa kuhusu mustakabali wa rasilimali za mafuta na gesi nchini, kwani muda wa mijadala mirefu sasa unakaribia kufikia mwisho.
Akizungumza wakati wa ziara yake katika kisima chenye historia ya utafutaji wa mafuta kilichopo Mkoa wa Magharibi, Waziri Masoud amesema kisima hicho kina historia ndefu na mchango mkubwa katika mchakato wa upatikanaji wa taarifa muhimu za kijiolojia, ambazo zinaweza kuongoza Zanzibar kufikia hatua ya uchimbaji.
#AzamTVUpdates
Mhariri | John Mbalamwezi