Jeshi la Polisi Tanzania linaendelea kutekeleza majukumu yake ya msingi ya kulinda maisha ya watu na mali zao sambamba na kuhakikisha hali ya amani, utulivu na usalama unaendelea kuimarika nchini.
Pia, limeendelea kuzuia uhalifu sambamba na kuwakamata wale wanaofanya makosa mbalimbali yakiwemo makosa ya kimtandao kama yale ya wanao endesha makundi mbalimbali katika mitandao ya kijamii ya kuhamasisha uhalifuna kuwachulia hatua kama sheria za nchi zinavyoelekeza.