Tom Barrack Mjumbe Maalumu wa Marekani nchini Syria amesema kuwa Washington ilijaribu mara mbili kupindua serikali ya Iran lakini iliambulia patupu.

Barrack ameeleza kuwa tangu mwaka 1964, Marekani imeongoza takribani mapinduzi 93 au majaribio ya “kubadili serikali” katika nchi mbalimbali duniani kote, yakiwemo mawili nchini Iran, ambayo hakuna hata moja lililofanikiwa.

Mjumbe huyo Maalumu wa Marekani nchini Syria ameeleza haya katika mahojiano aliyofanyiwa na kundi la habari la IMI Media lenye makao yake katika Umoja wa Falme za Kiarabu ambayo yalichapishwa Ijumaa iliyopita na gazeti la The National. 

Barrack ambaye pia ni Balozi wa Marekani nchini Uturuki amesema hayo miezi sita baada ya Marekani kuungana na kushirikiana na Israel kuishambulia Iran katikati ya mazungumzo ya nyuklia yaliyokuwa yakiendelea kati ya Washingoton na Tehran huko Oman.

Israel ilianzisha mashambulizi kinyume sha sheria dhidi ya Iran Juni 13 mwaka huu na kuua shahidi takriban watu 1,064 na kusambulia pia miundombinu ya kiraia.

Zaidi ya wiki moja baadaye, Marekani ilishambulia vituo vitatu vya nyuklia ya Iran yaani Fordow, Natanz na Isfahan ikikiuka pakubwa sheria za kimataifa.

Juni 24 mwaka huu, Iran ilifanikiwa kusimamisha hujuma hiyo ya jinai baada ya kufanya mashambulizi katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu (Israel).

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *