Vikosi vya usalama vya Benin vimezima jaribio la mapinduzi, huku hali ya mambo ikidhibitiwa. Haya yamebainishwa na Waziri wa Fedha Romuald Wadagni alipohojiwa na jarida la Jeune Afrique hii leo.

Mapema leo kundi la wanajeshi wa Benin lilitangaza kupitia kituo cha utangazaji cha serikali  kwamba limefanya mapinduzi na kumpindua Rais Patrice Talon, na wakat huo huo kumteua Luteni Kanali Pascal Tigri kuongoza kamati mpya ya kijeshi. 

Ubalozi wa Ufaransa nchini Benin pia ulisema katika taarifa yake kwamba milio ya risasi ilisikika katika kambi ya Camp Guezo, karibu na makazi ya rais.

Ubalozi huo uliwataka raia wa Ufaransa kusalia majumbani hadi itakapotolewa taarifa nyingine kuhusu hali ya mambo. 

Talon, mfanyabiashara wa zamani, amehudumu kama Rais wa Benin tangu mwaka 2016 na alichaguliwa tena kuiongoza nchi hiyo kwa muhula wa pili wa urais mwaka 2021.

Kundi la wanajeshi lililodai kumpindua Rais Talon lilisema kuwa mipaka nyoye nchini humo imefungwa na vyama vya kisiasa vimesimamishwa. 

Waziri wa Fedha wa Benin ameongeza kusema: “Tunasafisha mambo, lakini hayajaisha. Tuko salama. Romuald Wadagni ameeleza haya huku waliopanga jaribio la mapinduzi wakiendelea kushikilia nyadhifa zao. 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *