Waziri wa mambo ya ndani ya nchi George Simbachawene amesema maandamano yanayopangwa kufanyika kesho Desemba tisa hayakubaliki na ni haramu, kwani mpango huo haujulikani anayeuongoza na hakuna kibali kilichoombwa kwa Vyombo husika hivyo Jeshi la Polisi litawadhibiti wote watakaojaribu kutekeleza mpango huo.

Waziri Simbachawene amesema maandamano hayo yanayopangwa na kuhamasishwa kupitia mitandao ya kijamiini yasiyokuwa na ukomo, cha ajabu waandamanaji hao hawajafikisha sababu za kuwepo kwa mpango huo kwa jeshi la polisi lenye dhamana ya kuwalinda, hivyo akatumia fursa hiyo kuwaasa watanzania kutojihusisha na mpango huo.

Amesema kwa sasa hali ya usalama nchini ni shwari na inaendelea kuimarika baada ya kutokea kwa vurugu oktoba 29 zilizosababisha vifo, majeruhi na uharibifu wa mali za umma na za wananchi hivyo kamwe hatarajii kuona janga hilo lililogharimu maisha ya watu na mali zao likijirudia.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *