Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu, amesisitiza kuwa, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inapiga hatua na kusonga mbele licha ya kukabiliwa na mapungufu mengi.

Ayatullah Sayyid Ali Khamenei amesema hay oleo mbele ya hadhara kubwa ya maelfu ya maashiki wa Ahl-Bayti (as) na wasomaji wa tungo za kuwasifu Ahlul-Beiti wa Mtume (saw) kwa mnasaba wa maadhimisho ya kuzaliwa Bibi Fatima (as), binti ya Mtume Mtukufu (saw).

Kiongozi Muadhamu amesema, kuenea kwa dhana na utamaduni wa muqawama kutoka Iran hadi nchi nyingine katika eneo hili na hata nje yake ni ukweli ulio wazi na bayana.

Katika hafla hiyo iliyodumu kwa karibu masaa matatu, Imamu Khamenei alitoa mkono wa kheri, Baraka na fanaka kwa maadhimisho ya kuzaliwa Bibi Fatima (as), akisema: “Kwa muqawama wao wa kitaifa, watu wa Iran wamezuia njama mtawalia za adui za kubadilisha ‘utambulisho wa kidini, kihistoria na kitamaduni’ wa taifa hili. Leo, wakati ambapo lazima kuwe na maandalizi sahihi ya kujilinda na kushambulia ili kupinga propaganda na shughuli za vyombo vya habari za adui zinazolenga ‘akili, mioyo na imani’, Iran azizi inaendelea kusonga mbele licha ya matatizo na mapungufu yaliyopo kote nchini.”

Ayatullah Khamenei ameeleza kuwa, lazima tuwe Fatimiyuun na tufuate nyayo za mwanamke huyo ambaye ni kiigizo katika nyanja zote, ikiwa ni pamoja na kushikamana na dini, uadilifu, kujitahidi kufafanua ukweli, uhusiano mwema na mume, malezi ya watoto, na nyanja nyingine.

Akiashiria njama za zaidi ya karne moja za watumiaji mabavu wa kimataifa za kubadilisha utambulisho wa kidini, kihistoria na kitamaduni wa taifa la Iran, Ayatullah Khamenei amesema: Mapinduzi ya Kiislamu yamefelisha njama zote hizo na katika miongo ya hivi karibuni, taifa hili pia limezizuia kupitia muqawama, kusimama kidete na kutosalimu amri mbele ya mashinikizo ya kila upande kutoka kwa maadui zake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *