Serikali ya Marekani imeweka vikwazo vipya vinavyowalenga washirika wa rais wa Venezuela, pamoja na meli kadhaa zinazosafirisha mafuta yanayozalishwa nchini humo, Wizara ya Fedha imetangaza katika taarifa siku ya Alhamisi, Desemba 11. Wakati huo huo, rais wa Urusi ametangaza “uungwaji” wake kwa mwenzake wa Venezuela.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 3 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ametoa wito wa kuepukwa kwa hatua yoyote ambayo inaweza “kuvuruga” Venezuela na kada nzima. Siku ya Alhamisi jioni, kwenye televisheni ya kitaifa, Nicolas Maduro aliishutumu Marekani kwa “uharamia wa majini.”

Vikwazo hivi vipya vinawalenga wipwa watatu wa Nicolas Maduro, wawili kati yao waliachiliwa huru mwaka wa 2022 na Marekani kama sehemu ya kubadilishana wafungwa na Caracas, na pia meli sita zilizohusika katika kusafirisha mafuta ya Venezuela, ambazo kwa sasa ziko chini ya vikwazo vya Marekani.

Efrain Antonio Campo Flored na Franqui Francisco Flores de Freitas walihukumiwa mwaka wa 2017 kwa biashara ya dawa za kulevya baada ya kukamatwa nchini Haiti, ambayo iliwapeleka kwa mamlaka ya Marekani. Mpwa wa tatu anayelengwa, Carlos Erik Malpica Flores, ni naibu kiongozi wa kampuni ya mafuta inayomilikiwa na serikali ya Venezuela, Petroleos de Venezuela. Tayari alikuwa chini ya vikwazo vya Marekani kati ya 2017 na 2022.

“Nicolas Maduro na washirika wake wa uhalifu wanaingiza kwa wingia dawa za kulevya nchini Marekani, ambazo zinawatia sumu raia wetu. Chini ya uongozi wa Rais Trump, Wizara ya Fedha inawajibisha serikali (ya Venezuela) na washirika wake na makampuni kwa uhalifu wao,” amesema Waziri wa Fedha Scott Bessent, akinukuliwa katika taarifa kwa vyombo vya habari.

Mbali na wipwa watatu wa rais wa Venezuela, mfanyabiashara kutoka Panama, anayeshutumiwa kusaini mikataba mbalimbali na Nicolas Maduro na washirika wake, pia analengwa na vikwazo hivi vipya.

Washington inakusudia kunyakua mafuta kutoka kwa moja ya meli

Wakati huo huo, Washington inaongeza kuwa meli sita zinazoshutumiwa kushiriki katika usafirishaji wa mafuta ya Venezuela, ambazo zimekuwa chini ya vikwazo vya Marekani tangu 2019, sasa pia zinalengwa. Meli hizi zimesajiliwa nchini Uingereza, Visiwa vya Virgin vya Uingereza, na Visiwa vya Marshall.

Vikwazo hivi vinakuja huku Walinzi wa Pwani wa Marekani wakikamata meli ya mafuta usiku wa Jumatano kuamkia Alhamisi, wakituhumiwa kusafirisha mafuta ghafi ya Venezuela. Meli hii kwa sasa inaelekea bandari ya Marekani “ambapo Marekani inakusudia kukamata mafuta yake,” msemaji wa Ikulu ya White House Karoline Leavitt alisema katika mkutano na waandishi wa habari siku ya Alhamisi.

Rais wa Venezuela ameishutumu Marekani kwa “uharamia wa majini” siku ya Alhamisi jioni. “Waliwateka nyara wafanyakazi, wakaiba meli, na kuanzisha enzi mpya, enzi ya uharamia wa kihalifu wa majini huko Karibiani,” Nicolas Maduro ametangaza kwenye televisheni ya serikali.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres, “akiwa na wasiwasi” baada ya Marekani kukamata meli ya mafuta karibu na Venezuela, ametaka kuepuka hatua yoyote ambayo inaweza “kuvuruga utulivu wa Venezuela na kanda nzima,” mmoja wa wasemaji wake alisema siku ya Alhamisi, Desemba 11. “Tunatoa wito kwa wahusika wote kuepuka hatua yoyote ambayo inaweza kuongeza ongezeko la mvutano na kuvuruga utulivu wa Venezuela na kanda nzima,” Farhan Haq amewaambia waandishi wa habari, akitoa wito kwa “pande zote” kuheshimu sheria za kimataifa na Mkataba wa Umoja wa Mataifa.

Putin atangaza kumuunga mkono Maduro

Vladimir Putin ametangaza kumuunga mkono mwenzake wa Venezuela, Nicolas Maduro, katika simu siku ya Alhamisi, kufuatia uamuzi wa Marekani wa kukamata meli ya mafuta karibu na pwani ya Venezuela siku iliyotangulia.

Rais wa Urusi “alielezea mshikamano wake na watu wa Venezuela na akathibitisha tena kuunga mkono kwake sera za serikali ya Nicolas Maduro zinazolenga kulinda maslahi yake ya kitaifa na uhuru wake licha ya shinikizo la nje linaloongezeka,” Kremlin imesema katika taarifa ikiripoti mazungumzo ya simu, bila kutaja moja kwa moja Marekani.

Katika taarifa, Caracas imebainisha kwamba Vladimir Putin na Nicolas Maduro walikuwa na “mazungumzo muhimu ya simu, ambapo wakuu hao wawili wa nchi walithibitisha tena hali ya kimkakati, imara, na inayokua ya uhusiano wao wa pande mbili.”

Nicolas Maduro, mshirika wa karibu wa Vladimir Putin, alitangaza mwezi Mei uhusiano zaidi kati ya Moscow na Caracas kwa kusainiwa kwa mkataba wa ushirikiano.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *