#HABARI: Katika hali isiyotarajiwa, Waziri wa Wizara ya Ujenzi, Mh. Abdallah Ulega, amejikuta akitoa fedha ambazo kiasi chake hakikufahamika mara moja kama zawadi kwa Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Songwe, Mrakibu Mwandamizi wa Jeshi la Polisi (ASP) Joseph Bukombe, baada ya madereva katika Mpaka wa Tunduma, uliopo wilayani Momba, mkoani Songwe, kumuelezea Waziri Ulega, kuwa Afisa huyo wa Polisi amekuwa na msaada mkubwa baada ya kuja na ubunifu wa kuvusha magari katika Mpaka huo .
Waziri Ulega, amefika katika mpaka huo na kukagua miundombinu ya barabara kuzunguka Kituo hicho cha Forodha, kisha kusikiliza changamoto za madereva hao ambao wakati wakiwasilisha kero mbalimbali wakabainisha kuwa afisa huyo kwa kushirikiana na Maafisa wengine wa Polisi amekuwa sehemu muhimu ya kupunguza foleni hali ambayo iliyomvutia Waziri Ulega pamoja na viongozi wengine alioambatana nao kumpatia fedha kamanda huyo.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.