#HABARI: Wakili Hekima Mwasipu amesema Mteja wake Geoffrey Mwambe ameachiwa kwa dhamana na Jeshi la Polisi hapo jana Desemba 14,2025.

Mwambe ambaye aliwahi kuwa Waziri wa Viwanda na Biashara, anatuhumiwa kwa makosa mawili ya jinai ikiwemo kutuhumiwa kumtishia kumuua Kamanda Mkuu wa Polisi, ambaye hata hivyo hajatajwa jina lake na tuhuma za kiuchochezi za kimtandao.

Wakili Mwasipu amesema maombi ambayo yalitarajiwa kufanyika leo Jumatatu Desemba 15 ya kutoa amri ya dhamana au kuagiza Mwambe, afikishwe Mahakamani baada ya kudaiwa kushikiliwa na Polisi kwa zaidi ya siku nne bila kufikishwa Mahakamani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu hayana nguvu tena kwa sababu mteja wake yupo huru.

Kwa upande mwingine Wakili Mwasipu amesema Mwambe ataendelea kuripoti katika ofisi ya ZCO katika kipindi hiki ambacho upelelezi unaendelea na kama atabainika kuwa na kosa, basi atafikishwa Mahakamani.

Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *