
Mwanza. Tumia pesa Januari isikutishe. Mambo yapo huku yaani ni bata batani. Mwendo wa kufungua vizibo na kula bata hadi kuku waone wivu. Upo Mwanza? Zama maeneo haya ukale bata.
Saanane National Park
Kama wewe ni mdau wa Camping and Bonfire hakikisha mwisho wa mwaka huu, ukiwa Mwanza unatembelea Saanane National Park. Hiki ni kisiwa cha utalii. Utafanya na kuona mengi kama vile wanyama na mengineo.
Satosangara
Bata, ukiwa na familia zama Sato Sangara, huku utapata chakula cha asili ya Kanda ya Ziwa. Chimbo hili ukiwa na familia yako inapendeza zaidi. Hapa ni Restaurant, Bar na VIP Lounge ndani ya Rock City Mall.
The Cask, bar and Grill , Climix ,The kaffeehaous na Grand Prix
Kabla hujaondoka Rock City Mall tembelea The Cask, The Kaffehaus bila kusahau Climix na Grandprix eneo hili utakutana na michezo ya watoto pia.
Kwatunza , Club Elevet Malaika
Ukitaka sehemu ya vibe huku unakula upepo wa Ziwa Victoria pita KwaTunza ipo Ilemela ukiwa unaelekea Airport. Wazee wa kukesha mnaweza kutembelea Club Elevet Malaika hii ni night club ipo Ilemela pia.
Bundesliga Lounge
Watoto wa uswahilini huku ndio kwao sasa na bata la kufa mtu utawakuta Bundesliga Lounge kiwanja hiki kipo Nyasaka.
BonaSera, Tilapia
Wakishua zama Bona Sera ipo capri point mtaa huu pia kuna chaka jingine liitwalo Tlapia, Bonasera na Rockbeach Garden
Wagi Hill na Elly’s Beach
Kabla hujaondoka Mwanza pita Wag Hill ipo Nyegezi. Wale wa kupenda maji kama samaki kwenye beach kali zama Elly’s Beach ipo Nyanguge Magu.
Unakosaje kuinjoy na sikukuu hizi za mwisho wa mwaka fuatilia kila nakala zetu kwa mikoa tofauti upate kuzijua sehemu nyeti za kula bata msimu huu, unakaaje kinyonge sasa! Tule bata pamoja.