#HABARI: Wahitimu wa Chuo cha Ustawi wa Jamii (ISW) wametakiwa kuwa wabunifu na kubadilisha elimu ya huduma za ustawi kuwa biashara ili kujiajira wenyewe huku lengo kuu ni kutatua changamoto zilizopo ndani ya jamii zao.
Akizungumza katika Mahafali ya 49 ya Chuo cha Ustawi wa Jamii Kampasi ya Dar Es Salaam na Mahafali ya nane ya Kampasi ya Kisangara kwa niaba ya Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt. Dorothy Gwajima, Mkuu wa Wilaya Temeke, Sixtus Mapunda amewaasa kuitumikia taifa kwa utii na uadilifu.
“Mkawe wabunifu mkajiongeze dunia imebadilika mahitaji ya wananchi ni mengi
Elimu ya saikolojia haikuwa biashara kwasasa inahitajika sana katika jamii zetu na mnapata fedha hivyo tuhamishie huduma za ustawi wa jamii kuwa biashara kuna makampuni na taasisi wanahitaji huduma hizi tuwe na juhudi na kuna matokeo ya juhudi za muda mrefu,” amesisitiza Mhe. Mapunda
Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wanawake na Makundi Maalum Amon Mpanju amesema wahitimu hao katika fani mbalimbali za huduma za ustawi wa jamii watatumika kuisaidia jamii kutatua changamoto zao katika kuleta Ustawi wao.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
📱Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 📱kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.