#HABARI: Mahamana Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam imeamuru Kampuni ya UDA Rapid Transport Ltd kumlipa fidia ya Sh. milioni 88.8 Frank Zebaza, baada ya kugongwa na basi la mwendokasi, ambapo pia imebainika kuwa Dereva Hafidhi wa Ally alikuwa akiendesha basi hilo kwa mwendo hatarishi ambaye pia Mahakama imemuamuru kumlipa Frank fidia ya shilingi Milioni kumi.
Hukumu hiyo ilitolewa Desemba 19, 2025 na Jaji Griffin Mwakapeje, kufuatia kesi ya madai namba 28992 ya mwaka 2024 iliyofunguliwa na Zebaza dhidi ya UDA Rapid Transport Ltd, dereva Hafidhi Ally, Shirika la Taifa la Bima (NIC) na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), akidai fidia ya jumla ya Sh. milioni 600 kwa madhara aliyopata.
Katika madai yake, Zebaza aliomba alipwe Sh. milioni 350 kama fidia maalumu kwa gharama za matibabu na matumizi mengine yanayohusiana na ajali hiyo, Sh. milioni 150 kama fidia ya jumla kwa maumivu na mateso pamoja na Sh. milioni 100 kama fidia ya adhabu.
Akisoma hukumu hiyo, Jaji Mwakapeje alisema ushahidi uliowasilishwa mahakamani unaonesha wazi kuwa mlalamikaji alipata majeraha makubwa yaliyomlazimu kufanyiwa upasuaji mkubwa na hadi sasa anaendelea kukumbwa na athari za kudumu katika mfumo wa fahamu na hisia, hali iliyosababisha kupungua kwa uwezo wake wa kufanya kazi.
“Majeraha haya yalimlazimu mlalamikaji kuhama kutoka Mbezi Makondeko kwenda Mikocheni kwa sababu za usalama na uangalizi wa kiafya.
“Aidha, ameshindwa kuendelea na shughuli zake za awali kama mwanamuziki na mpishi, hivyo kupoteza uwezo wake wa kujipatia kipato,” alisema Jaji Mwakapeje.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.