MWIMBAJI maarufu wa nyimbo za Injili nchini Tanzania, Ambwene Mwasongwe, amewapa mashabiki na Watanzania ujumbe wa faraja na matumaini, akisisitiza umuhimu wa kumtegemea Mungu katika kila hatua ya maisha.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Mwasongwe aliandika ujumbe ulioigusa mioyo ya wengi, akieleza kuwa bila msaada wa Mungu hakuna mwanadamu anayeweza kusaidia kwa ukamilifu, lakini mara Mungu anaposaidia hakuna cha kuogopwa wala kinachoweza kushinda.
“Mungu asipotusaidia hakuna atakayetusaidia. Ila Mungu akitusaidia hakuna wa kututisha wala kutushinda. Nakuombea uzima, afya na amani unapojiandaa kuvuka mwaka huu,” aliandika Ambwene. SOMA: Rose Muhando afunika Mtoko wa Pasaka
Ujumbe huo umepokelewa kwa hisia chanya na mashabiki wengi, ambao wameendelea kumpongeza kwa kutumia jukwaa lake kueneza maneno ya matumaini, imani na upendo, hususan katika kipindi hiki cha mabadiliko ya mwaka.
