#HABARI: Mahakama ya Wilaya ya Pangani, mkoani Tanga, imetoa hukumu ya kifungo cha miaka 30 jela kwa mtuhumiwa Grayson Muze Msem…#HABARI: Mahakama ya Wilaya ya Pangani, mkoani Tanga, imetoa hukumu ya kifungo cha miaka 30 jela kwa mtuhumiwa Grayson Muze Msem…

#HABARI: Mahakama ya Wilaya ya Pangani, mkoani Tanga, imetoa hukumu ya kifungo cha miaka 30 jela kwa mtuhumiwa Grayson Muze Msemo (55), Mkristo, mkazi wa Raskazoni – Tanga, baada ya kupatikana na hatia ya kosa la kubaka mtoto mwenye umri wa mwaka 1 na miezi 4.

Awali imeelezwa mahakamani hapo kuwa mtuhumiwa alitenda kosa hilo mnamo tarehe 1 Septemba 2025 katika eneo la Funguni Street, Pangani.

Akisoma hukumu hiyo Mheshimiwa Husna Mwiula, Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Pangani, amesema kuwa Mahakama imeridhika na ushahidi uliowasilishwa na kumhukumu mtuhumiwa kifungo cha miaka 30 jela ili iwe fundisho kwa jamii na kuhakikisha haki inatendeka.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *