#HABARI: Watu wanne wanaosadikiwa kuwa ni majambazi wamefariki dunia wakati wakipatiwa matibabu baada ya kujeruhiwa katika majibizano ya risasi na Jeshi la Polisi mkoani Songwe. Tukio hilo lilitokea katika eneo la Ilembo, wilayani Mbozi, wakati askari walipokuwa wakijaribu kuwatia nguvuni watuhumiwa hao waliokuwa wamejificha ndani ya nyumba. Awali, kundi hilo linadaiwa kuvamia duka la simu na huduma za kifedha la Bwana Gabriel Nsemwa lililopo ndani ya KITUO cha Mabasi cha Vwawa, ambapo walimuua mlinzi William Mwampashi kwa kitu chenye ncha kali na kupora fedha pamoja na simu.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe, SACP Augustino Senga, amethibitisha kuwa tukio hilo la uvunjaji na mauaji lilitokea alfajiri ya Disemba 30, 2025. Kamanda Senga ameeleza kuwa, licha ya kufanikiwa kuwapata watuhumiwa hao wanne, Jeshi la Polisi bado linaendelea na msako mkali dhidi ya washiriki wengine wa uhalifu huo ambao inasemekana wamekimbilia mikoa ya jirani.

Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *