#HABARI: Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino imeanza rasmi zoezi la upimaji wa ardhi katika Kata za Buigiri na Chamwino, likiwa na lengo la kurasimisha umiliki wa ardhi, kulinda vyanzo vya maji na kupunguza migogoro inayohusiana na ardhi katika maeneo hayo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, Tito Mganwa, amesema zaidi ya hekari 1,000 zinatarajiwa kupimwa katika awamu ya kwanza ya zoezi hilo, ambalo limepangwa kufanyika kwa kuzingatia misingi ya kisheria na mpango wa maendeleo wa mji wa Chamwino.
Amesema sambamba na utekelezaji wa zoezi hilo, Halmashauri inaendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhusu umuhimu wa upimaji na urasimishaji wa Ardhi ili kuhakikisha wananchi wanamiliki maeneo yao kihalali na kisheria.
Baadhi ya wakazi wa kata ya Buigiri wamepongeza hatua hiyo, wakisema imekuja wakati muafaka na itasaidia kuondoa migogoro ya ardhi, kudhibiti ujenzi holela na kuwezesha matumizi bora ya ardhi kwa maendeleo ya jamii.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
-
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.