Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Adam Malima, amewataka wananchi waliokuwa wakitarajia kuwapokea ndugu zao waliokuwa wakisafiri kutoka Morogoro Desemba 31, 2025, lakini hawajawaona, kutoa taarifa katika ofisi za Wakuu wa Wilaya au Ofisi ya Mkuu wa Mkoa.

Hatua hiyo imelenga kusaidia zoezi la uchunguzi na utambuzi wa vinasaba vya miili ya waliopoteza maisha katika ajali ya barabarani iliyotokea usiku wa kuamkia mwaka mpya mkoani humo.

Ajali iliyohusisha basi dogo la abiria lililokuwa likitoka Morogoro kuelekea Mombo mkoani Tanga, ambalo liligongana na lori la mizigo na kusababisha moto mkali.

✍Theresia Mwanga
Mhariri | @claud_jm

#AzamTVUpdates

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *