Watu wenye ulemavu ambao ni wakazi wa mkoa wa njombe wametaja changamoto tano zinazowapa ugumu wa maisha ikiwemo kutengwa, masharti magumu ya mikopo ya asilimia kumi, Kutoshirikishwa katika vikao vya maamuzi kutokana na kukosa uwakilishi katika baraza la madiwani pamoja na kudharauliwa, jambo wamelitaja kama linawapa ugumu katika kuiona thamani yao.
Wamezitaja changamoto hizo katika risala maalumu waliyoiwasilisha mbele ya mbunge wa viti maalumumu mkoa wa njombe Sigrada Mligo (𝗖𝗛𝗔𝗨𝗠𝗔) Aliye waalika katika chakula cha pamoja kama sehemu ya kutambua uwepo wao sambamba na kuwasikiliza kero zao.
Kiongozi wa chama cha walemavu mkoa wa njombe Alfred Msigwa amesema moja kati ya mambo yanayowapa ugumu ni pamoja na kutengwa/kutopata ushirikishwaji wa karibu katika vikao vya maamui hususani kwa mambo yanayowahusu watu wenye ulevu.
Kando na changamoto hizo walizozitaja, vile vile wametoa mipango yao ya mwanzo wa mwaka 2026 kuwa ni pamoja na kutembelea shule zote za wanafunzi wenye mahitaji maalumu kabla ya shule kufunguliwa ili waweze kuwasikiliza na waone namna bora ya kuwasaidia.
Mbunge Sigrada mligo amewakabidhi fedha taslimu kama sehemu ya bajeti ya kukamilisha ziara yao katika shule zenye mahitaji maalumu huku akiahidi kwenda kuziwasilisha bungeni changamoto zote walizoainisha ili ziweze kupatiwa ufumbuzi wa haraka.
Hata hivyo Sigrada ameihamasisha jamii kushikamana na kuwasaidia watu wenye ulemavu akiwataja kuwa wao pia ni sehemu ya jamii hivyo wanahitaji upendo na kujaaliwa kama bin Adam wengine.